Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ameonya kuhusu kitisho cha matumizi ya nguvu yanayoweza kufanywa na wafuasi wafuasi wa makundi ya kigaidi. Hali ya usalama ni tete nchini Ujerumani amesema kansela Angela Merkel alipotembelea kituo cha pamoja cha idara za usalama za Ujerumani cha kinga dhidi ya ugaidi mjini Berlin. Kansela Merkel amesema idadi ya visa vinavyotishia usalama "imeongezeka mno". Wakati huo huo kansela Merkel amewahaakikishia maafisa wa idara za usalama uungaji mkono wa serikali. Katika kituo cha idara za usalama cha kinga dhidi ya ugaidi, idara 40 zinazohusika na masuala ya usalama zinabadilishana maarifa. Kituo hicho cha usimamizi kilichoundwa mwaka 2004 kinashughulikia hatari inayotokana na wafuasi wa dhehebu la Sunni wa itikadi kali ya dini ya kiislamu, ambao wanafuata misingi ya mafunzo ya kiislamu ya Saudia arabia.
Mwisho wa habari/ 291